BALOZI WA MAREKANI NCHINI AMUAGA RASMI WAZIRI WA ULINZI NA JKT

BALOZI WA MAREKANI NCHINI AMUAGA RASMI WAZIRI WA ULINZI NA JKT

  • Habari
  • January 13, 2025
  • No Comment
  • 87

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 13, January, 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake wa uwakilishi nchini Tanzani, Balozi Michael Anthony Battle, SR, katika Ofisi ndogo za Wizara ya Ulinzi na JKT, Upanga, jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho Dkt. Tax amemhakikishia Balozi Battle, kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Marekani katika masuala yenye manufaa kwa nchi hizo mbili na wananchi wake.

Naye Balozi wa Marekani aliyemaliza muda wake nchini, Michael Battle, akizungumza katika kikao hicho na Waziri wa Ulinzi amesema nchi yake na Balozi ajaye wa Marekani Tanzania, itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano na Tanzania na kuahidi kuwa Marekani inaiona Tanzania kama mshirika mkubwa wa kimkakati katika ushirikiano wa maendeleo.

Ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ya Marekani na kuongeza kuwa ni matarajio yake kuwa kupitia majadiliano mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika yatasaidia nchi yake kuibua kwa undani maeneo muhimu ambayo Serikali ya Tanzania inahitaji kuendelea kushirikiana na Marekani.

Tanzania na Marekani zimekuwa zikishirikiana katika nyanja za Afya, kupitia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Shirika la Misaada la USAID, Elimu, Kilimo, Biashara na uwekezaji, pamoja na masuala ya Ulinzi na Usalama.

Kikao hicho kati ya Waziri Stergomena Tax na Balozi Battle, kilihudhuriwa pia na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Andrew Lentz, pamoja na maafisa waandamizi toka Ubalozi wa Marekani nchini na wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ya Tanzania.

Related post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *