CCM YAJA NA SULUHISHO LA KUDUMU LA MAJI ILALA NA SEGEREA

CCM YAJA NA SULUHISHO LA KUDUMU LA MAJI ILALA NA SEGEREA

  • Habari
  • September 30, 2025
  • No Comment
  • 19
13 / 100 SEO Score

 MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesema chama hicho kikipewa ridhaa ya kuongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo, kitahakikisha changamoto ya maji katika Wilaya ya Ilala na Jimbo la Segerea inabaki kuwa historia.

Amesema azma ya CCM ni kuanzisha mradi mkubwa wa uzalishaji na usambazaji maji kwa maeneo hayo, sambamba na kupanua mtandao wa mabomba ili kufikisha huduma kila sehemu.

Aidha, mabomba yaliyoharibika au kukatika chini ya ardhi yatafukuliwa na kuwekwa mapya ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama.

Dk. Nchimbi ameongeza kuwa Serikali ya CCM itajenga tanki kubwa la maji kwa ajili ya Jimbo la Segerea, ambapo kwa sasa lina ujazo wa mita za mraba 273 pekee, lakini litaboreshwa na kuongezwa mara nne hadi kufikia ujazo wa mita za mraba 845 milioni.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Jimbo la Segerea, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Dk. Nchimbi alisema hatua hiyo inalenga kutatua kero kubwa inayowakabili wakazi wa maeneo hayo kwa muda mrefu.

Pamoja na mambo mengine,Dkt.Nchimbi alipata nafasi ya kuwanadi Wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea,Ndugu Bonnah Kamoli pamoja na Madiwani

Related post

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza mitungi ya gesi 19,530…
SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kuanza utekelezaji wa awamu mpya ya ujenzi wa minara 280 ya mawasiliano,…
TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *