DKT.MZEE:MRADI WA  MARKUP II KUONGEZA THAMANI YA MAZAO NA AJIRA

DKT.MZEE:MRADI WA  MARKUP II KUONGEZA THAMANI YA MAZAO NA AJIRA

  • Habari
  • October 15, 2025
  • No Comment
  • 11
23 / 100 SEO Score
Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Dkt. Said Seif Mzee, amesema utekelezaji wa mradi wa uongezaji thamani katika mazao ya kimkakati kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi (MARKUP II), utaongeza ukuaji wa mnyororo wa thamani katika uzalishaji na kuchochea ongezeko la ajira.

Dkt.Mzee ameyasema hayo leo Oktoba 15,2025 jijini Dodoma wakati akifungua  Mkutano wa tatu wa Taifa wa kamati ya Makatibu Wakuu wa Mradi wa MARKUP II, ulioandaliwa kwa lengo la kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya miaka minne (2023–2027) kwa kushirikiana na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa MARKUP ni matokeo ya mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza (MARKUP I), ambayo licha ya mafanikio, pia yalibaini changamoto zilizotumika kuboresha utekelezaji wa awamu hii,” amesema Dkt.Mzee.

 

Aidha amesema mradi huo unahusisha fursa za masoko na uwezo wa kuyafikia masoko ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi, hasa kwa sekta ya viwanda vidogo vinavyotoa mchango mkubwa katika ajira na uchumi wa nchi wanachama wa EAC.

 

“Kama tulivyokubaliana katika mkutano wetu wa Februari 2025 jijini Dodoma, awamu hii imelenga kuimarisha uongezaji thamani katika mazao ya kahawa, ngozi, parachichi, viungo vya chakula na vinywaji, pamoja na masuala ya vifungashio,” ameongeza.

Hata hivyo , Dkt.Mzee amesema  kupitia mkutano huo, wajumbe wamepokea taarifa kuhusu maandalizi ya mkutano wa makatibu wakuu wa kikanda utakaofanyika Bunjumbura, Burundi kuanzia Novemba 3–5, 2025, ambapo maazimio ya mkutano wa Dodoma yatakuwa msingi wa majadiliano hayo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Market Access Upgrade Programme (MARKUP II) kutoka ITC, Bw. Safari Fungo, amesema kuwa  mradi huo unatekelezwa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.

Aidha amefafanua kuwa lengo la mradi huo ni kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao mbalimbali katika nchi wanachama wa EAC, ambapo kwa upande wa Tanzania, umejikita katika mazao ya kahawa, bidhaa za ngozi na vifungashio.

 

 

 

 

 

 

 

Related post

SERIKALI YAPANGA KUIMARISHA UBORA NA USALAMA WA  CHAKULA

SERIKALI YAPANGA KUIMARISHA UBORA NA USALAMA WA  CHAKULA

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza…
RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA HASARA

RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA…

11 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile Musa amesema mafunzo yanayotolewa…
BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *