DKT NCHIMBI ATOA AHADI YA MATUMIZI YA NDEGE NYUKI ‘DRONES’ | ILI KUFUKUZA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO

DKT NCHIMBI ATOA AHADI YA MATUMIZI YA NDEGE NYUKI ‘DRONES’ | ILI KUFUKUZA WANYAMA WAHARIBIFU WA MAZAO

  • Habari
  • October 18, 2025
  • No Comment
  • 8
13 / 100 SEO Score

Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia CCM, Balozi Emmanuel Nchimbi amesema Serikali ijayo ya Chama hicho inakusudia Kutumia ndege nyuki ‘Drones’ kwa ajili ya kufukuza Wanyama waharibifu katika kata ya Mwaya, Kilombero ili mazao ya wakulima yabaki kuwa Salama.

Dkt Nchimbi ametoa hakikisho hilo leo Oktoba 18, 2025 akiwa katika mkutano wa Kampeni za Urais, ambao umefanyika katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Pamoja na mambo mengine ,Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo kumuombea kura za ushindi wa kishindo mgombea Urais wa chama hicho,Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilombero Ndugu Abubakar Damian ASENGA,pamoja na mgombea Ubunge wa jimbo la Mlimba Ndugu Kellen Rose RWAKATARE na Madiwani.

Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 25 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.

Related post

WAFANYABIASHARA, WAJASIRIAMALI HANDENI WAFUNGUKA SABABU ZA KUJITOKEZA KUPIGA KURA OKTOBA 29

WAFANYABIASHARA, WAJASIRIAMALI HANDENI WAFUNGUKA SABABU ZA KUJITOKEZA KUPIGA KURA…

18 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score   Na Augusta Njoji, Handeni TC Makundi mbalimbali ya wananchi katika…
REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza mitungi ya gesi 19,530…
SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kuanza utekelezaji wa awamu mpya ya ujenzi wa minara 280 ya mawasiliano,…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *