
KENYA YAWATAKA RAIA WAKE KUREJEA MAKWAO
- Habari
- February 21, 2025
- No Comment
- 83
Kutokana na kuongezeka kwa ghasia nchini Kongo kati ya vikosi vya usalama na waasi wa M23, Serikali ya Kenya imetoa wito kwa wananchi wake kuondoka mapema na kurejea makwao.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi ikiwa ni siku chache baada ya waasi wa M23 kudhibiti miji ya Bukavu na Goma, huku taarifa zikidai tayari waasi wameukaribia mji unaopakana na Burundi wa Uvira.
Wakati huo jumuiya ya Kimataifa imesisitiza kusitishwa kwa vita hivyo na kurejeshwa kwa hali ya amani, katika maeneo yote ya mashariki mwa DRC.
✍️| @kastulelias_