
LISSU AMBURUZA VIBAYA MBOWE UCHAGUZI CHADEMA
- Habari
- January 22, 2025
- No Comment
- 71
Baada Ya Kusubiriwa Kwa Hamu Zaidi Juu Ya Nani Atakalia Kiti Cha Umwenyekiti Ndani Ya Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Hatimaye, Aliyekua Rais Wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika Tls Tundu Lissu, Ametangazwa Kuwa Mwenyekiti Mpya Wa Chama Hicho.
Lissu Amechaguliwa Baada Ya Kupata Kura 513 Sawa Na Asilimia 52.5 Zilizopigwa Na Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Wa Uchaguzi Wa Chama Hicho Alfajiri Ya Leo Januari 22, 2025, Huku Mbowe Akipata Kura 482 Na Odero Kura.
Kabla Ya Uchaguzi Huo Lissu Alikua Makamu Mwenyekiti Wa Chadema, Ambapo Alikuwa Akichuana Vikali Na Aliyekua Mwenyekiti Freeman Mbowe Ambaye Alikuwa Akitetea Kiti Hicho Pamoja Na Odero Charles Odero.
Kupitia Mtandao Wa X, Mbowe Amempongeza Lissu Na Wengine Wote Walioaminiwa Na Kupewa Jukumu La Kuiongoza Chadema, Na Kuwatakia Heri Katika Kukipeleka Mbele Chama Hicho.
✍️| Kastul Elias