
MBOWE AKUBALI YAISHE CHADEMA
- Habari
- January 22, 2025
- No Comment
- 83
Aliyekua Mwenyekiti Wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe, Amekubali Kushindwa Na Mpinzani Wake Tundu Lissu Katika Uchaguzi Wa Kumchagua Mwenyekiti Wa Chama Hicho Upande Wa Tanzania Bara.
Mbowe Ambaye Amekua Madarakani Kwa Miongo Miwili Akikiongoza Chama Hicho Kikuu Cha Upinzani Nchini Tanzania Amekiri Kushindwa Katika Uchaguzi Huo Licha Ya Kuwa Matokeo Bado Hayajatangazwa Mpaka Hivi Sasa.
Kupitia Mtandao Wa X, Mbowe Amekiri Wazi Kuwa Ameshindwa Katika Uchaguzi Huo Na Amempongeza Lissu Na Kumtakia Kila Lakheri Katika Kukisimamia Chama Hicho Na Kuhakikisha Kinazidi Kusonga Mbele.
Mpaka Hivi Sasa Matokeo Ya Uchaguzi Huo Hayajatajwa Na Tunakuahidi Kukujuza Kila Litakalotokea.
✍️| Kastul Elias