
MKUU WA JESHI LA ISRAEL AJIUZULU
- Habari
- January 22, 2025
- No Comment
- 75
Meja Jenerali Herzi Halevi Ambaye Alikua Ni Mkuu Wa Jeshi La Israel Amejiuzulu Wadhifa Huo Kutokana Na Kile Alichokiita “Uzembe Katika Majukumu Yake” Baada Ya Kushindwa Kuzuia Uvamizi Wa Kundi La Wanamgambo Wa Hamas, Oktoba 7 Mwaka 2023.
Katika Barua Ya Kujiuzulu Meja Jenerali Halevi Amesema Amefikia Uamuzi Wa Kujiudhulu Wadhifa Huo Kwasababu Alishindwa Kuzuia Uvamizi Wa Oktoba 7 Na Kusema Kwamba Anaondoka Katika Wakati Ambapo Yamepatikana Mafanikio Katika Jeshi Hilo La Israel.
Wakati Huo, Kiongozi Wa Upinzani Wa Israel Yair Lapid Ameitaka Serikali Ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu Ijiuzulu Baada Ya Halevi Kujiuzulu.
✍️| Kastul Elias
Chanzo: DW