
MNYAMA KUREJEA KILELENI LEO?
- Michezo
- February 6, 2025
- No Comment
- 67
Baada Ya Kuwashuhudia Jana Wananchi Yanga Wakitoa Kipigo Cha Mabao 6-1 Dhidi Ya Kengold Na Kukwea Kileleni Mwa Msimamo Wa NBC, Leo Jioni Wekundu Wa Msimbazi Simba Sc, Watakua Uwanjani Kucheza Na Fountain Gate.
Mchezo Huo Utachezwa Katika Uwanja Wa Tanzanite Kwaara Uliopo Manyara Majira Ya Saa 10 Jioni, Ambapo Simba Watakua Na Kazi Moja Tu Ya Kuhakikisha Wanapata Alama Tatu Zitakazowafanya Kurudi Kileleni Mwa Msimamo Huo.
Si Mara Ya Kwanza Kwa Simba Kukutana Na Fountain Gate Kwani Mchezo Wa Kwanza Walipokutana Katika Uwanja Wa KMC Complex, Simba Iliibuka Na Ushindi Wa Magoli 4-0.
✍️| Kastul Elias