MWANDUMBYA ATOA RAI KWA MAAFISA MASUULI KUBORESHA UKUSANYAJI MAPATO YASIYO YA KODI

MWANDUMBYA ATOA RAI KWA MAAFISA MASUULI KUBORESHA UKUSANYAJI MAPATO YASIYO YA KODI

  • Habari
  • September 19, 2025
  • No Comment
  • 21
15 / 100 SEO Score

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya akiongoza Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilicholenga kujadili na kubuni mbinu za kisasa za kuboresha ukusanyaji wa Kodi, Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Na. Peter Haule na Joseph Mahumi, WF, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya ametoa rai kwa Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kuendelea kutekeleza majukumu yao ya ukusanyaji wa mapato kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ikiwemo suala la uwasilishaji wa mapato ya Serikali katika Mfuko Mkuu wa Serikali kwa wakati.

Bw. Mwandumbya ametoa rai hiyo wakati wa kufunga Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma

Bw. Mwandumbya alisema kuwa wajumbe wa Kikao hicho wanatakiwa kusimamia matumizi sahihi ya mifumo ya kielektroniki likiwemo suala la matumizi ya control number jumuishi, kufanya kazi kwa weledi bila kutumia mabavu au kukusanya ada na tozo bila kutoa huduma iliyokusudiwa.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo, kutawezesha kuondoa kero na kuweka mazingira mazuri na rafiki ya ulipaji kodi kwa hiyari baina ya walipa kodi.

Kikao hicho kililenga kujadili na kubuni mbinu za kisasa za kuboresha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya Kodi ili kuwezesha nchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo bila utegemezi mkubwa kwa nchi wahisani.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya akiongoza Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilicholenga kujadili na kubuni mbinu za kisasa za kuboresha ukusanyaji wa Kodi, Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera Wizara ya Fedha, Dkt. Jonson Nyella, akieleza umuhimu wa mapato yasiyo ya kodi kwa maendeleo ya nchi, wakati wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha anayesimamia Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya akifunga  Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilicholenga kujadili na kubuni mbinu za kisasa za kuboresha ukusanyaji wa Kodi, Kikao kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Tume ya Madini, CPA Idfonce Masoud, akieleza mchango wa sekta ya madini katika mapato yasiyo ya kodi, wakati wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Tume ya Umwagiliaji, Dkt. Consolatha Kapinga, akieleza mchango wa sekta ya umwagiliaji katika mapato yasiyo ya kodi, wakati wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mapato na Uwekezaji, Bw. Leonard Msafiri, akieleza mchango wa sekta ya ardhi katika mapato yasiyo ya kodi, wakati wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kutoka Wizara ya Fedha, wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi, wakifuatilia mada kuhusu ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi wakati wa Kikao cha Maafisa Masuuli wanaohusika na ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kilichofanyika Ukumbi wa Kambarage Wizara ya Fedha, Treasure Square, jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Dodoma)

Related post

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza mitungi ya gesi 19,530…
SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kuanza utekelezaji wa awamu mpya ya ujenzi wa minara 280 ya mawasiliano,…
TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *