
NANI KUCHUKUA KITI CHADEMA LEO?
- Habari
- January 21, 2025
- No Comment
- 76
Wanachama Wa Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo (CHADEMA) Leo Wana Kazi Nzito Ya Kumchagua Mwenyekiti Wa Chama Hicho Upande Wa Tanzania Bara.
Mwenyekiti Wa Sasa Freeman Mbowe Atakua Na Kazi Nzito Ya Kutetea Kiti Chake Hicho Mbele Ya Aliyewahi Kuwa Mbunge Wa Singida Mashariki Kupitia Chama Hicho Tundu Lissu.
Nafasi Ya Umwenyekiti Wa CHADEMA Katika Uchaguzi Huu, Inagombaniwa Na Watu Watatu; Tundu Lissu, Freeman MBowe Na Odero Charles Odero.
Wataalamu Wa Siasa Wanasema Mchuano Mkali Kati Ya Hao Watatu Ni Ule Wa Tundu Lissu Aliyewahi Kuwa Rais Wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Pamoja Na Freeman Mbowe Ambaye Amehudumu Ndani Ya Chama Hicho Akiwa Mwenyekiti Kwa Zaidi Ya Miaka 20.
Wababe Hao Wawili Katika Siasa Za Chadema Wamekua Wakicharuana Wakati Wa Kampeni Zao Kila Mmoja Akitaka Apate Kiti Hicho, Na Leo Majibu Ya Nani Atakua Mwenyekiti Yatapatikana.
✍️| Kastul Elias