
PAPA FRANCIS KUENDELEA KUKAA HOSPITALI
- Habari
- February 16, 2025
- No Comment
- 59
Hali ya kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis, inaendelea kuimarika baada ya kukimbizwa hospitalini kwa matibabu ya haraka kufuatia kupata maambukizi kwenye njia ya upumuaji.
Shirika la habari la Italia, ANSA limeripoti kuwa Papa Francis amelazwa katika hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Rome na anapokea matibabu na hivyo hatoweza kujitokeza hadharani hii leo Jumapili kuongoza ibada ya wiki kwa sababu madaktari wamemtaka kiongozi huyo wa Kanisa katoliki apumzike.
Aidha, Taarifa ya makao makuu ya kanisa Katoliki, Vatican imesema Papa Francis ataendelea kuwa hospitalini kwa muda kwa ajili ya kupokea matibabu.
✍️| Kastul Elias