
SIKU YA KONDOMU KUADHIMISHWA DODOMA
- Habari
- February 12, 2025
- No Comment
- 72
Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP), Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) na Shirika la Aids Healthcare Foundation (AHF) kwa pamoja wataadhimisha siku ya Kondomu Duniani kwa mara ya kwanza nchini Februari 13, 2025.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari, Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP), Dkt. Zeye Nkomela amesema maadhimisho hayo yatafanyika mkoani Dodoma.
Chanzo: Swahili Times