
WATU SABA WAPOTEZA MAISHA MLIPUKO WA BOMU SUDAN
- Habari
- May 4, 2025
- No Comment
- 65
Watu wasiopungua saba wameuawa na wengine 20 wajeruhiwa kufuatia mashambulizi ya mabomu katika mji wa Old Fangak, nchini Sudan Kusini.
Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limethibitisha kuwa Katika mashambulizi hayo, hospitali na duka la dawa la MSF vilivyokuwa vituo pekee vya huduma za afya katika Kaunti ya Fangak vimeharibiwa kabisa.
Kwa mujibu wa MSF, bomu la kwanza lilidondoshwa moja kwa moja kwenye duka la dawa na kuliteketeza kwa moto, likisababisha uharibifu mkubwa kwa hospitali jirani.
Video iliyopatikana kutoka kwa mashahidi wa tukio hilo inaonyesha wakaazi wa eneo hilo wakikimbilia eneo la tukio wakiwa na ndoo za maji wakijaribu kuzima moto katika duka la dawa la MSF