
WAZIRI WA ULINZI NA JKT ZIARANI NCHINI ITALIA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ULINZI WA ITALIA
- Michezo
- March 27, 2025
- No Comment
- 70
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 26, Machi, 2025, amefanya ziara ya kikazi nchini Italia kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Ulinzi wa Italia Bwana Guido Crosetto.
Mazungumzo baina ya Viongozi hao wa Serikali za Tanzania na Italia yaligusa pia maeneo muhimu ya ushirikiano katika Sekta ya Ulinzi baina ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Italia kupitia wizara yake ya Ulinzi.