
YANGA USO KWA USO NA PAMBA JIJI LEO NBC
- Michezo
- February 28, 2025
- No Comment
- 86
Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga, jioni ya leo watakua na kibarua kizito cha kuhakikisha wanazipata alama tatu mhimu mbele ya wenyeji wao Pamba Jiji FC.
Mchezo huo utakaochezwa majira ya saa 10 jioni katika dimba la CCM Kirumba, huku Pamba wakiingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya Yanga, katika mchezo wa raundi ya kwanza ya NBC.
Mbali na mchzo huo, Walina Asali, Tabora United nao watashuka uwanjani majira ya saa 8 mchana kucheza na Dodoma Jiji FC, katika mwendelezo wa NBC. Mchezo huo utachezwa katika dimba la Ally Hassan Mwinyi lililopo mkoani Tabora.
✍️| @kastulelias_