
EBITOKE AKAMATWA NA JESHI LA POLISI UFUKWENI MTWARA
- Burudani
- August 1, 2025
- No Comment
- 47
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limethibitisha kumkamata Msanii wa vichekesho nchini Tanzania, Anastanzia Exavery Mahatane (27) maarufu kama Ebitoke katika fukwe za Msanga Mkuu akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa, kinyume na madai aliyoyatoa mtandaoni kuwa ametekwa na kutumbukizwa shimoni.
Taarifa ya Jeshi la Polisi, imesema kuwa Ebitoke amekua akiishi Mkoani Mtwara tangu Aprili 2025 na alikuwa akiishi kwa watu aliowafahamu, huku Uchunguzi wa awali umebaini kuwa hakutekwa kama alivyoeleza kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 30.
Aidha, Jeshi la Polisi limemfikisha katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara kwa matibabu, na limewaomba ndugu na jamaa zake kufika kumsaidia au kumchukua.