
AZAM FC YAWEKA KAMBI ARUSHA
- Michezo
- August 1, 2025
- No Comment
- 40
KIKOSI cha Azam FC kimewasili salama Arusha kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya(pre-season) chini ya benchi jipya la Ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Mkongo Jean-Florent Ibenge.
Tayari Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imesema msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, 2025/2026 unatarajiwa Septemba 16, mwaka huu 2025 – wastani wa wiki mbili tu baada ya kumalizika kwa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
Msimu mpya wa Ligi Kuu umelazimika kuchelewa kutokana na Tanzania mwenyeji mwenza wa CHAN pamoja na jirani zake, Kenya na Uganda zinazotarajiwa kuanza Agosti 2 hadi 30, mwaka huu.