NEMC IPO VIWANJA VYA NANENANE DODOMA- MAONESHO YA WAKULIMA

NEMC IPO VIWANJA VYA NANENANE DODOMA- MAONESHO YA WAKULIMA

  • Habari
  • August 1, 2025
  • No Comment
  • 49
13 / 100 SEO Score
Na.Mwandishi Wetu.
BARAZA  la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma, likitoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira kupitia kilimo rafiki kwa mazingira.
Kupitia banda lake, NEMC inatoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya mazingira, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (TAM) kabla ya kuanzisha miradi ya kilimo, ujenzi na shughuli nyingine za kiuchumi.

Aidha, elimu nyingine inayotolewa ni kuhusu,Katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki,Athari za uchafuzi wa vyanzo vya maji,Umuhimu wa kuzingatia kilimo hifadhi,Ulipaji wa ada za mazingira kwa mujibu wa sheria na Elimu ya urejelezaji wa taka kwa ajili ya kulinda mazingira na kuongeza kipato.

Maonesho ya Nanenane mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.” NEMC imesisitiza kuwa uchaguzi wa viongozi wenye maono katika sekta hizo ni msingi wa utekelezaji wa sera na sheria za mazingira kwa maendeleo endelevu.

Baraza hilo limewahimiza wakulima, wafugaji, wavuvi na wananchi wote wanaotembelea maonesho hayo kutembelea banda la NEMC ili kupata elimu sahihi juu ya mbinu bora za kilimo na uzalishaji zinazozingatia utunzaji wa mazingira.

“Ustawi wa kilimo na uchumi wetu unategemea sana afya ya mazingira yetu. Tunawahamasisha wananchi kufika kujifunza na kushirikiana nasi katika kulinda mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho,” imesema NEMC.

Maonesho ya Nanenane kitaifa yameanza rasmi Agosti 1 na yanatarajiwa kufikia kilele chake Agosti 8, 2025.

Related post

SERIKALI YAPANGA KUIMARISHA UBORA NA USALAMA WA  CHAKULA

SERIKALI YAPANGA KUIMARISHA UBORA NA USALAMA WA  CHAKULA

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza…
RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA HASARA

RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA…

11 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile Musa amesema mafunzo yanayotolewa…
BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *