
SON ATANGAZA KUONDOKA TOTTENHAM HOTSPUR
- Michezo
- August 2, 2025
- No Comment
- 54
Baada ya kuhudumu kwa miaka 10, Nahodha wa Tottenham Son Heung-min amesema kuwa ataondoka katika klabu hiyo majira haya ya joto.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Korea Kusini alijiunga na Spurs akitokea Bayer Leverkusen mwaka 2015 na amefunga mabao 173 katika mechi 454.
Son mwenye umri wa miaka 33, ambaye yuko chini ya mkataba na Spurs hadi 2026, yuko kwenye mazungumzo na Klabu ya Los Angeles inayoshiriki Ligi Kuu nchini Marekani.
Son ameelezea uamuzi huo kama uamuzi mgumu zaidi ambao ameufanya katika maisha yake ya soka.
“Nilikuja London kaskazini nikiwa mtoto, nikiwa na umri mdogo sana, mvulana mdogo alikuja London ambaye hata hakuzungumza Kiingereza, Kuondoka kwenye klabu hii kama mtu mzima ni wakati wa kujivunia sana.” Son alisema.
“Nahitaji mazingira mapya ya kujipa changamoto. Nahitaji mabadiliko kidogo, miaka 10 ni muda mrefu,” Son aliongeza. “Nilitumia muda mwingi kutafakari kama nilitaka kupata uzoefu wa soka katika mazingira tofauti.”
Tottenham wako Seoul kama sehemu ya maandalizi yao ya kabla ya msimu mpya, Son ataanza na nahodha wa timu dhidi ya Newcastle katika mechi yao ya kirafiki siku ya Jumapili, ikimaanisha kuwa mechi yake ya mwisho katika klabu hiyo inaweza kuchenzwa nchini mwake.