
P. DIDDY NA JAY – Z WAFUTIWA MASHITAKA MAREKANI
- Burudani
- February 15, 2025
- No Comment
- 99
Rapa Sean Diddy Combs maarufu kama P Diddy na mwenzake Jay – Z wamefutiwa mashitaka ya ubakaji yaliyokuwa yakiwakabili, baada ya mwanamke aliyewashtaki kwahiari yake kuondoa kesi hiyo mahakamani.
Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Jane Done aliwasilisha mahakamani kesi hiyo akidai kuwa alifanyiwa mkasa huo miaka 25 iliyopita na P. Diddy baada ya tafrija ya Tuzo za Muziki za MTV mwaka 2000, akiwa na umri wa miaka 13.
Lakini baadae pia Done alimwongeza rapa Jay – Z akidai kuwa nay eye siku ya tukio alikuwepo na kwamba alihusika katika kumdunga dawa za kulevya na baadae kumfanyia tukio la ubakaji.