
TANI 1500 ZA PLASTIKI ZATEKETEZWA NCHI NZIMA
- Habari
- March 24, 2025
- No Comment
- 87
Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira NEMC limesema litaendelea na kampeni zake za mitaa kwa mitaa katika kuhamasisha na kuzuia madhara ya matumizi ya mifuko ya Plastiki.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo Immaculate Semesi jijini Dodoma, wakati akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya Baraza hilo katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa awamu ya sita na kuongeza kuwa mifuko ya plastiki imesababisha adha nyingi katika jamii.
Immaculate ameongeza kuwa Baraza limefanikiwa kuandaa vipindi 88 vya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari na mikutano 20 ya wadau kuhusu madhara ya matumizi ya mifuko ya plastiki na kufanya kaguzi katika maeneo 178 ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki, ambapo maeneo 57 yalikutwa na makosa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.
Aidha, katika Kaguzi hizo zaidi ya tani 150 za vifungashio visivyokidhi viwango vilikamatwa, vikataifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria.
NEMC imetoa rai kwa Wananchi, taasisi na serikali kuwa suala la udhibiti wa vifungashio vya plastiki ni la Taifa nzima hivyo ni vyema kila mwananchi akashiriki katika zoezi hilo kwaajili ya kuleta matokeo chanya.