
AHOUA ANAONGOZA MBIO ZA MFUNGAJI BORA MSIMU HUU
- Michezo
- May 9, 2025
- No Comment
- 53
Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Jean Charles Ahoua amezidi kujiweka katika nafasi nzuri kuelekea katika mbio za kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa NBC msimu huu baada ya hapo jana kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 5-1 walioupata Simba dhidi ya Pamba Jiji FC.
Ahoua sasa amefikisha mabao 15 kwenye mbio za ufungaji bora akimshusha straika wa Yanga, Clement Mzize mwenye mabao 13, huku Prince Dube na Leonel Ateba wakiwa na mabao 12 kila mmoja.
MVP huyo wa msimu uliopita katika Ligi ya Ivory Coast yupo kwenye mazingira mazuri ya kushinda kiatu cha ufungaji kutokana na kuwa na faida ya mchezo mmoja mkononi.
Mpaka sasa vinara wa upachikaji mabao wa NBC ni hawa hapa:
🇨🇮 Jean Ahoua: 1️⃣5️⃣
🇹🇿 Clement Mzize: 1️⃣3️⃣
🇿🇼 Prince Dube: 1️⃣2️⃣
🇨🇲 Ateba: 1️⃣2️⃣
🇬🇭 Jonathan Sowah: 1️⃣1️⃣
🇰🇪 Elvis Rupia: 1️⃣0️⃣