
AJALI YA NDEGE YAUA WATU 20 SUDAN KUSINI
- Habari
- January 30, 2025
- No Comment
- 79
Mamlaka ya anga ya Sudan Kusini imesema kuwa, ndege hiyo iliyokuwa ikitokea jimbo la Unity kwenda mji mkuu wa Juba, ilikua imebeba watu 21 na ilipata hitilafu na kuanguka muda mfupi baada ya kupaa na kusababisha vifo vya watu 20.
Mamlaka hiyo imeongeza kuwa abiria waliofariki katika ajali hiyo ni raia wa sudan pamoja na wageni ambao walikua wafanyakazi wa makampuni ya mafuta waliokuwa wanarudi nyumbani baada ya kufanya kazi kwenye visima vya mafuta.
Bado haijajulikana ni nini kilisababisha ajali hiyo na serikali ya jimbo la Unity ilisema inafanya kazi na makampuni ya mafuta na kampuni ya ndege kubaini majina ya wahanga katika ajali hiyo.
Ajali za ndege katika taifa la sudan zimekua zikitokea mara kwa mara kutokana na mashirika ya ndege kutumia ndege za zamani na zisizo na matengenezo bora lakini pia ubovu wa barabara nao unatajwa kuwa chanzo cha ajali hizo.
✍️| Kastul Elias