MALAWI YAZUIA BIDHAA ZA KILIMO ZA TANZANIA

MALAWI YAZUIA BIDHAA ZA KILIMO ZA TANZANIA

  • Habari
  • April 17, 2025
  • No Comment
  • 14

Serikali imetangaza kuwa itazuia uingizaji wa mazao na bidhaa zote za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini kufikia siku ya Jumatano ijayo, iwapo nchi hizo hazitabadilisha msimamo wao wa kuweka vikwazo dhidi ya bidhaa za kilimo kutoka Tanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na kuongeza kuwa licha ya jitihada za kidiplomasia na mawasiliano na Waziri wa Kilimo wa Malawi, bado hakuna majibu yoyote rasmi, na hivyo serikali inalazimika kuchukua hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa ndani.

“Ni vyema ifahamike kuwa kwa kipindi cha miaka mitano, Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kufungua soko la ndizi nchini Afrika Kusini bila mafanikio. Hali hii inafanana na changamoto tulizopitia kwa zaidi ya miaka kumi katika kufungua soko la parachichi, hadi pale tulipoamua kuchukua hatua za kulinda maslahi ya nchi yetu,”

Hatua hiyo inafuatia taarifa rasmi kuwa Serikali ya Malawi imezuia uingizwaji wa bidhaa kadhaa za kilimo kutoka Tanzania, ikiwemo unga, mchele, tangawizi, ndizi na mahindi, hatua iliyosababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaosafirisha bidhaa hizo.

Related post

WATU SABA WAPOTEZA MAISHA MLIPUKO WA BOMU SUDAN

WATU SABA WAPOTEZA MAISHA MLIPUKO WA BOMU SUDAN

Watu wasiopungua saba wameuawa na wengine 20 wajeruhiwa kufuatia mashambulizi ya mabomu katika mji wa Old Fangak, nchini Sudan Kusini.  …
TANZANIA NA MALAWI ZASAINI MAKUBALIANO KUENDELEA NA BIASHARA

TANZANIA NA MALAWI ZASAINI MAKUBALIANO KUENDELEA NA BIASHARA

Nchi za Tanzania pamoja na Malawi zimekubaliana kuendelea na biashara kuanzia Mei 02, 2025 kufuatia kikao cha Mawaziri wa Mambo ya…
SIMBA SC KUZISAKA ALAMA TATU LEO MKOANI KIGOMA

SIMBA SC KUZISAKA ALAMA TATU LEO MKOANI KIGOMA

Wana Fainali wa Kombe la Shirikisho 2025, Klabu ya Simba leo watashuka katika uwanja wa Lake Tanganyika uliopo mkoani Kigoma kucheza…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *