
SERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UCHUJAJI DAMU
- Habari
- March 19, 2025
- No Comment
- 67
Serikali Kupitia Bohari ya Dawa (MSD) inatekeleza mpango maalumu wa kuongeza upatikaji wa huduma ya uchujaji damu (dialysis), ikiwa ni sehemu matibabu ya figo ili kupunguza gharama za huduma hiyo.
Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa kwa kiasi kikubwa, serikali imewekeza kiasi cha shilingi Bilioni 7.7 ambapo idadi ya mashine zinazotumika katika uchujaji wa damu imeongezeka kutoka mashine 60 na kufikia mashine 137 katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Jumla ya hospitali 11 kote nchini zimeanza kutumia machine hizo kutoa huduma kwa wenye uhitaji ikiwemo hospitali za Rufaa za mikoa ya Amana, Mwananyamala, Temeke, Morogoro, Katavi, Tumbi, Chato, Sekoe Toure na UDOM Hospitali.
Aidha, mkakati huu umelenga kupunguza idadi gharama zinazotozwa kutokana na huduma hiyo kutoka kati ya shilingi laki 2 hadi shilingi laki 2 na nusu kwa ‘session moja’ hadi kufikia kiasi cha chini ya shilingi laki moja.