SHAMBULIO LA DRONI LAUA WAPALESTINA 10 TAMUN

SHAMBULIO LA DRONI LAUA WAPALESTINA 10 TAMUN

  • Habari
  • January 30, 2025
  • No Comment
  • 77

Wizara Ya Afya Ya Palestina Imesema Shambulio La Droni Lililotekelezwa Na Israel Katika Kijiji Cha Tamun Kilichopo Ukingo Wa Magharibi Limesababisha Vifo Vya Watu 10.

 

Israel Haijakiri Wazi Kuhusika Katika Shambulio Hilo Lakini Imesisitiza Azma Yake Ya Kusitisha Shughuli Za Shirika La Kuhudumia Wakimbizi Wa Kipalestina UNRWA Kuanzia Leo, Ikilishtumu Shirika Hilo La Umoja Wa Mataifa Kujaza Wanachama Wa Hamas.

 

Wakati Huo, Rais Wa Marekani Donald Trump Anatarajiwa Kutia Saini Amri Ya Rais Kuhusu Chuki Dhidi Ya Wayahudi, Ambayo Inaelezwa Kuwalenga Hasa Wanafunzi Walioshiriki Maandamano Ya Kuwaunga Mkono Wapalestina Wakati Wa Vita Vya Gaza.

 

Amri Hiyo Imesababisha Makundi Ya Haki Za Raia Kutoa Wasiwasi Kwamba Itaingilia Haki Za Uhuru Wa Kujieleza Na Inaweza Kukumbana Na Pingamizi Za Kisheria.

 

Maandamano Hayo Yalizuka Kama Jibu Kwa Mzozo Wa Gaza Na Yamejumuisha Ongezeko La Vitendo Vya Chuki Dhidi Ya Wayahudi, Waislamu, Waarabu, Na Watu Wa Asili Ya Mashariki Ya Kati.

✍️| Kastul Elias

Related post

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza mitungi ya gesi 19,530…
SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kuanza utekelezaji wa awamu mpya ya ujenzi wa minara 280 ya mawasiliano,…
TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *