
TLS YALAANI VITENDO VYA UDHALILISHAJI DHIDI YA LISSU
- Habari
- August 1, 2025
- No Comment
- 34
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kimelaani vitendo wanavyodai ni udhalilishaji na ukandamizaji vinavyofanywa na Jeshi la Magereza dhidi ya Mwanachama wao, Wakili Tundu Lissu wakati shauri lake likiendelea Mahakamani.
TLS imesema vitendo anavyofanyiwa vinakiuka Katiba ya Tanzania na Mikataba ya Kimataifa inayolinda haki, na utu wa kila Mtu.
TLS imeomba kukutana na Jaji Mkuu kujadili suala hilo na kulitaka Jeshi la Magereza kuacha mara moja vitendo hivyo, ikiwemo kuzuia askari wasiotambulika kuingia mahakamani na kuwachukulia hatua askari wote waliohusika katika shambulio dhidi ya Lissu, Julai 30, 2025.
Chama hicho kimesema iwapo mambo haya hayataheshimiwa, Uongozi wa TLS hautasita kuchukua hatua za dharura kulinda hadhi za Wanachama wake na Haki Jinai Nchini ili kutuma ujumbe wa wazi na thabiti dhidi ya ukiukwaji wa haki za Wakili yeyote.
Credit: Jamii Forums