
WAHAMIAJI WASIO NA VIBALI KUPELEKWA GUANTANAMO
- Habari
- January 30, 2025
- No Comment
- 107
Kufuatia Amri Ya Kuwaondoa Raia Wote Wanaoishi Bila Vibali, Rais Wa Marekani, Donald Trump, Ametangaza Mipango Ya Kuandaa Kituo Cha Kuwazuia Wakimbizi Hao Katika Gereza La Kijeshi La Guantanamo.
Vyama Vya Wafanyakazi Wa Serikali Nchini Marekani Vimewashauri Wanachama Wake Kuwa Makini Na Utawala Wa Trump Na Kupendekeza Mpango Wa Kujitolea Kujiuzulu Mpango Ambao Utawawezesha Wafanyakazi Kujiuzulu Kwa Malipo Ya Mshahara Wa Miezi Minane.
Wakati Huo Rais Wa Cuba, Miguel Diaz-Canel, Ameielezea Mipango Hiyo Kuwa Ya Ukatili, Akidai Kuwa Wakimbizi Hao Watawekwa Karibu Na Vituo Vilivyotumika Kwa Mateso Na Vifungo Vinavyokiuka Sheria.
Kituo Hicho, Ambacho Ni Tofauti Na Gereza Hilo Lenye Ulinzi Mkali, Kiliwahi Kutumika Miaka Ya Nyuma Kuhifadhi Wakimbizi, Wakiwemo Wahaiti Na Wacuba Waliokamatwa Baharini Na Kitakua Na Uwezo Wa Kupokea Wahamiaji Elfu 30.
✍️| Kastul Elias