
WAZIRI JAFO AAGIZA MSAKO MKALI KARIAKOO
- Habari
- May 7, 2025
- No Comment
- 65
Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jaffo ametoa maelekezo ya kufanyika kwa msako wa kubaini wanaofanya biashara bila kufuata taratibu za Kisheria kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo Mei 7, 2025.
Jaffo ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Soko la Kariakoo na kueleza kuna ukiukwaji wa Sheria za Nchi unaofanywa na Wageni kwa kushirikiana na wazawa, kwa kufanya biashara bila kuwa na vibali vinavyotakiwa.
Mnamo Aprili 16, 2025 ziliibuka tuhuma kutoka kwa wadau ambao pia walitoa wito kwa Serikali kuweka mifumo madhubuti ya kudhibiti, kusimamia na kuelekeza uwekezaji wa kigeni ili kuhakikisha kuwa faida za uwekezaji huo zinawanufaisha Watanzania wengi Zaidi.