
MGOGORO WA MAREKANI NA CHINA WACHUKUA SURA MPYA
- Habari
- April 17, 2025
- No Comment
- 75
Kufuatia mgogoro wa kibiashara na Marekani, China imepunguza ununuzi wa mafuta kutoka Marekani kwa asilimia 90 na kuanza kuagiza kiasi kikubwa cha mafuta kutoka katika Taifa la Canada.
Uagizaji wa mafuta ya Marekani kwenda China umeshuka kwa kiasi kikubwa kutoka mapipa milioni 29 mwezi Juni, 2024 hadi milioni 3 mwezi huu.
Mvutano wa kibiashara kati ya mataifa haya mawili ulizuka baada ya Rais wa Marekani kutangaza kuweka kodi katika bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka China lakini umeingia katika siku mbaya baada ya Trump kuongeza kodi hiyo hadi asilimia 245 kwa bidhaa zote za Uchina.