AFRIKA KUSINI YAONDOA WANAJESHI WAKE DRC
- Habari
- February 27, 2025
- No Comment
- 96
Taarifa iliyotolewa jana na jeshi la Afrika Kusini ilisema kuwa, jumla ya wanajeshi 127 wa nchi hiyo wameondolewa kutoka mstari wa mbele wa mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku wanne kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Msemaji wa jeshi hilo, Prince Tshabalala, amesema Taifa hilo lilituma wanajeshi zaidi ya 1,000 nchini Kongo, kukiongoza kikosi cha SADC chenye wanajeshi pia kutoka Malawi na Tanzania ambapo kati yao wanajeshi 21 walirejea nyumbani siku ya Jumanne (Februari 25) na wengine 106 walirudi Jumatano (Februari 26)
Afrika Kusini imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake, tangu kuuawa kwa wanajeshi wake 14 mwishoni mwa mwezi Januari katika majibizano ya risasi a Wanamgambo wa M23 wanaotajwa kuungwa mkono na Rwanda.
✍️| @kastulelias_
