
BOTI YAWAKA MOTO NA KUUWA WATU TAKRIBANI 50
- Habari
- April 17, 2025
- No Comment
- 51
Watu wasiopungua 50 wamefariki dunia na wengine takribani 100 hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakiitumia kusafiri kuwaka moto na kupinduka kwenye Mto Congo, karibu na Mji wa Mbandaka, Kaskazini Maghariribi.
Akizungumza na Shirika la Habari la AFP, Kamishna wa Mto Congo, Competent Loyoko, amesema ajali hiyo ilitokea Aprili 15, 2025, huku chanzo cha ajali hiyo ni Mtu mmoja aliyekuwa akipika kwenye Boti hiyo ambayo ilikuwa imebeba takribani watu 400.
Ajali hiyo ya boti sio ya kwanza kutokea katika Nchi hiyo ya Afrika ya Kati, ikumbukwe mwezi Desemba 2024 Watu 38 walifariki baada ya Kivuko kuzama na Oktoba 2024 boti moja ilizama katika Ziwa Kivu, na kuua Watu 78.