
CHRIS BROWN ADAI FIDIA YA TSH TRION 1.2 KWA KUCHAFULIWA
- Burudani
- January 23, 2025
- No Comment
- 175
Mwanamuziki Wa Marekani Chris Brown Amewasilisha Kesi Dhidi Ya Kampuni Ya Filamu, Warner Bros. Discovery, Kwa Madai Kuwa Kampuni Hiyo Ilichapisha Taarifa Za Uongo Na Zinazomdhalilisha Kupitia ‘Documentary’ Ya “Chris Brown: A History Of Violence”.
Katika Kesi Hiyo Brown Ameitaka Kampuni Hiyo Kumlipa Kiasi Cha Tsh. Trilioni 1.2, Kwa Kumchafua Bila Kujali Madhara Ambayo Yangempata.
Mwanasheria Wake, Levi Mccathern Amesema “Kesi Hii Ni Kuhusu Kulinda Ukweli, Licha Ya Kupewa Ushahidi Kuwa Taarifa Hizo Si Za Kweli Bado Kampuni Hiyo Iliandaa ‘Documentary’ Hiyo Na Kuichapisha Kwa Makusudi Wakifahamu Wako Kinyume Na Majukumu Yao Kama Waandishi Wa Habari.”
Documentary Ya Chris Brown A History Of Violence Inamuonesha Mwanamuziki Huyo Sambamba Na Mwanamuziki Mwenzake P Diddy Aliyekizuizini Hadi Sasa Wakiwa Na Mwanamke Ambaye Inaelezwa Kuwa Chris Brown Alimdharirisha Baada Ya Kumpa Pombe Kali.
✍️| Kastul Elias