DRC YAPIGA MARUFUKU NDEGE ZA RWANDA KUTUMIA ANGA LAKE
- Habari
- February 12, 2025
- No Comment
- 81
Serikali ya Jamhuri ya Kongo imepiga marufuku ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa Rwanda au kwingineko lakini zenye makao yake nchini Rwanda kuruka juu ya anga ya DRC.
Hatua hiyo imefikiwa na serikali ya Kinshasa kufuatia vita vya kichokozi vilivyosababisha vifo vya watu 3,000 huko Goma ambapo Rwanda imekua ikituhumiwa na serikali ya Rais Tshisekedi kuhusika moja kwa moja katika vita hiyo.
Hata hivyo, Wachambuzi wanasema hatua hii itakuwa pigo kwa Rwanda kutokana na ukubwa wa anga ya Kongo, lakini wanahoji ni namna gani serikali ya Kinshasa itaweza kutekeleza hatua hiyo.