
IRAN YASEMA VITISHO VYA ISRAEL BADO VINAENDELEA
- Habari
- August 3, 2025
- No Comment
- 39
Kamanda Mkuu wa jeshi la Iran Amir Hatami amesema leo kuwa vitisho kutoka kwa Israel bado vinaendelea, akisisitiza kuwa Tehran iko tayari kujibu kwa nguvu iwapo uchokozi utaanzishwa upya.
Hatami ameongeza kuwa Iran haipaswi kumdharau adui akimaanisha Israel na kufikiria vitisho vyake vimekwisha.
Kamanda Mkuu huyo wa jeshi la Iran ameeleza kwamba nguvu ya makombora na droni ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu inasalia imara na tayari kwa oparesheni.
Mnamo mwezi Juni, Israel na Marekani zilifanya mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran wakati wa kile kinachojulikana kama vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran.
Mwezi uliopita, waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz alionya kwamba nchi yake itaishambulia tena Iran iwapo itatishiwa usalama wake.