
SAFARI YA STARS CHAN 2024 KUANZA LEO
- Michezo
- August 2, 2025
- No Comment
- 54
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itashuka dimbani leo saa 2:00 usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi B na wa ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024 kumenyana na Burkina Faso.
Mashindano haya ya CHAN yanafanyika kwa mara ya kwanza kwa ushirikiano wa nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda.
Stars imepangwa Kundi B lenye timu kama Burkina Faso, Mauritania, Madagascar na Afrika ya Kati, huku Kenya wao wakipangwa Kundi A pamoja na DR Congo, Morocco, Angola na Zambia. Wakati huo Uganda yeye akipangwa C lenye timu kama Algeria, South Africa, Guinea, Niger na Uganda.