
SIMBA SC KUIVAA MBEYA CITY KESHO CRDB CUP
- Michezo
- April 12, 2025
- No Comment
- 15
Hatua ya robo fainali ya Kombe la CRDB Bank Federation Cup itaanza kutimua vumbi kesho jumapili ambapo Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watawaalika Mbeya City mchezo utakaochezwa katika dimba la KMC, Mwenge Jijini Dar es Salaam.
Mbali na hapo siku ya jumatatu ya Aprili 14, 2025 JKT Tanzania watawaalika Pamba Jiji huku Singida Black Stars wakitafuta nafasi ya kutinga nusu fainali ya kombe hilo kwa kucheza na Kagera Sugar.
Hatua ya robo fainali itatamatishwa na mchezo kati ya mabingwa tetezi wa michuano hiyo, Klabu ya Yanga ambao watachuana vikali na wapiga debe wa Shinyanga, Stand United siku ya jumanne ya Aprili 15, 2025 katika dimba la KMC Complex.