
WAKULIMA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA MIKOPO NAFUU YA TIB
- Habari
- March 20, 2025
- No Comment
- 66
Wakulima kote nchini wametakiwa kutumia fursa kwa kuomba mikopo katika Benki ya Maendeleo nchini (TIB), ili kukuza miradi yao uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Lilian Mbassy, jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya benki hiyo katika kipindi cha miaka minne ya utawala wa awamu ya sita wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mbassy amesema lengo kubwa la benki hiyo ni kuhakikisha inatoa mitaji ya kati na ya muda mrefu yenye masharti nafuu kwa wakulima na wafanyabiashara kote nchini huku dhamana ikiwa ndiyo kigezo pekee kinachozingatiwa wakati wa utoaji wa mikopo hiyo.
Katika hatua nyingine, Mbassy amesema benki hiyo hutoa muda zaidi kwa mkopaji ambaye amepata hasara katika mradi wake kutokana na majanga ya asili ikiwemo ukame.