
WATAHINIWA 67 WAFUTIWA MATOKEO NECTA
- Habari
- January 23, 2025
- No Comment
- 70
Baraza La Mitihani La Tanzania (NECTA) Limetangaza Kuwa Limewafutia Matokeo Watahiniwa 67 Waliofanya Udanganyifu Wakati Wa Mtihani Wa Taifa Wa Kidato Cha Nne Uliofanyika Mwezi Novemba Mwaka 2024.
Akitangaza Matokeo Hayo Mkoani Dar Es Salaam, Katibu Mtendaji Wa NECTA Dkt. Said Mohammed Amesema Katika Idadi Hiyo Wamo Wanafunzi Watano Waliandika Lugha Ya Matusi Katika Karatasi Zao Za Mtihani Wa Kidato Cha Nne.
Aidha, Baraza La Mitihani La Tanzania Limezuia Kutoa Matokeo Ya Watahiniwa 459 Ambao Walipata Matatizo Ya Kiafya Na Kushindwa Kufanya Mtihani Wa Kidato Cha Nne 2024 Kwa Masomo Yote Au Idadi Kubwa Ya Masomo.
Watahiniwa Husika Wamepewa Fursa Ya Kufanya Mtihani Mwaka 2025 Kwa Masomo Ambayo Hawakuyafanya Kwa Sababu Ya Ugonjwa Kwa Mujibu Wa Kifungu Cha 32(1) Cha Kanuni Za Mitihani.
Pia, NECTA Imekifungia Kituo Cha P6384 BSL Open School Kilichopo Mkoa Wa Shinyanga Kuwa Kituo Cha Mitihani Ya Taifa Kutokana Na Kuratibu Mipango Ya Udanganyifu.
Kituo Hicho Kinafungiwa Kwa Mujibu Wa Kifungu 4(8) Cha Kanuni Za Mitihani Mwaka 2016 Hadi Hapo Baraza Litakapojiridhisha Kuwa Ni Salama Kwa Uendeshaji Wa Mitihani Ya Taifa.