
WAUWAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI NA POLISI KIGOMA
- Habari
- August 1, 2025
- No Comment
- 34
Watu watatu wanaosadikika kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano na askari wa Jeshi la Polisi baada ya kunaswa wakijaribu kuteka magari ya abiria yanayotoka Kigoma kuelekea mikoa mingine.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, ACP Filemon Makungu, amesema majambazi hao walikuwa wakilenga kuwapora maki abiria mbalimbali zikiwemo simu, fedha taslimu na vitu vingine vya thamani, kabla ya kuingia kwenye mtego wa polisi.
Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Kigendeka, Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma ambapo taarifa ya Jeshi la Polisi imeongeza kuwa, silaha mbili zimekamatwa katika tukio hilo, ikiwemo bunduki aina ya AK-47 na nyingine ya kutengenezwa kienyeji, ambazo majambazi walikuwa wakizitumia kutekeleza uhalifu wao.