YANGA SC YATINGA RAUNDI YA PILI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

YANGA SC YATINGA RAUNDI YA PILI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  • Michezo
  • September 27, 2025
  • No Comment
  • 26
11 / 100 SEO Score

KLABU ya Yanga SC ya Tanzania imetinga raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) baada ya ushindi wa jumla wa mabao 5-0 dhidi ya Williete SC kutoka  nchini Angola.

Yanga SC ilianza kampeni yake kwa kishindo baada ya kushinda mabao 3-0 ugenini nchini Angola, kabla ya kumaliza kazi nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kwa ushindi wa mabao 2-0.

Katika mchezo wa marudiano uliofanyika  leo Jumamosi, Septemba 27, 2025, mabao ya Yanga yalifungwa na Pacôme Zouzoua dakika ya 70 na  bao la pili limefungwa na Aziz Andabwile dakika ya 86, na kuwanyanyua  mashabiki  kwa  furaha ya kuendelea na safari ya Afrika.

Kwa ushindi huo, Yanga SC sasa itachuana na Silver Strikers ya Malawi katika raundi ya pili. Silver Strikers imelitinga hatua hiyo kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Elgeco Plus ya Madagascar kwenye mchezo wa kwanza, kisha kulazimisha suluhu tasa ya 0-0 kwenye marudiano nyumbani Malawi.

Yanga SC italazimika kuwa makini zaidi hatua inayofuata, huku lengo lao kubwa likiwa ni kufika hatua ya makundi na kuendeleza historia katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Related post

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

REA YAANZA KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI 19,530 MKOANI MARA

14 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza mitungi ya gesi 19,530…
SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

SERIKALI KUPITIA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI*.

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatarajia kuanza utekelezaji wa awamu mpya ya ujenzi wa minara 280 ya mawasiliano,…
TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

TANZANIA YAJIPANGA KUONGOZA AFRIKA KATIKA MKUTANO WA COP30

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *