
KIONGOZI WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA AUWAWA ECUADOR
- Habari
- February 15, 2025
- No Comment
- 84
Polisi nchini Ecuador imesema kuwa Kanali Porfirio Cedeno, aliyekuwa kiongozi wa kikosi maalamu cha anga cha kupambana na mtandao wa wauza dawa za kulevya amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha.
Tukio hilo limetokea kwenye mji ulioathiriwa vibaya na uhalifu unaotokana na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya wa Guayaquil, ambapo Cedeno alikuwa anasafiri kutoka mji huo kwenda mji Manta kwenye hafla moja ya kijeshi na ndipo watu hao walipolimiminia gari lake risasi zaidi ya 20 na kumuua papo hapo.
Wakati huo, Waziri wa Ulinzi wa Ecuador Gian Carlo Loffredo amesema mauaji ya Cedeno yanapaswa kujibiwa kwa vita kali dhidi ya magenge ya uhalifu.