
UNFPA YASITIKITISHWA NA MAREKANI KUSITISHA UFADHILI WAKE
- Habari
- May 11, 2025
- No Comment
- 22
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Afya ya Uzazi na Jinsia (UNFPA) limetangaza kuwa Serikali ya Marekani imeamua kusitisha ufadhili wake wa baadaye kwa shirika hilo, hatua inayotajwa kusitisha msaada muhimu kwa Mamilioni ya Watu walio katika Mazingira ya Migogoro na kwa Wakunga wanaookoa Maisha ya akina Mama wakati wa kujifungua
Imeelezwa Marekani imefikia hatua hiyo ikidai UNFPA inahusishwa na utoaji wa Mimba wa kulazimishwa na upasuaji wa Uzazi wa hiari Nchini China, madai ambayo yamekanushwa mara kadhaa na tathmini huru, ikiwemo zile zilizofanywa na Serikali ya Marekani yenyewe
Uamuzi huu unakuja huku zaidi ya ruzuku 40 za kibinadamu zikiwa tayari zimesitishwa, zenye thamani ya takriban Dola Milioni 335. UNFPA ilikuwa ikitegemea wastani wa Dola Milioni 180 kutoka Marekani kwa kila mwaka.