
WANAOPIGA MZIKI KUPITA KIASI WAONYWA
- Burudani
- March 24, 2025
- No Comment
- 95
Baraza la Taifa la Uhifadhi wa Mazingira NEMC limetoa onyo kwa wamiliki wa kumbi za starehe (Baa) nchini kuhakikisha wanafuata sheria za utunzaji wa mazingira.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza hilo Immaculate Swale, wakati akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya Baraza hilo katika kipindi cha miaka minne cha awamu ya sita ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo amesema wataendelea kuwatafta kwa kushirikiana na jeshi la polisi na kuwafikisha katika mamlaka husika ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.
Immaculate amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki wa kumbi hizo kupiga mziki Kupitia kiasi Hali inayosababisha mtetemo mkubwa na kusababisha kero kwa Wananchi hasa wanaoishi maeneo jirani na kumbi hizo, ambapo Katika kipindi cha miaka minne (4), jumla ya kaguzi 9,606 zilifanyika na malalamiko 1,483 yalishughulikiwa hasa katika eneo la kelele na mitetemo.
Aidha, pia amewataka wamiliki wa vyombo vya moto, Makanisa na Misikiti kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria za utunzaji wa mazingira ili kutokusabisha kero kwa wakazi wa karibu na maeneo hayo.