WAWEKEZAJI WA MIGODI HANDENI WATAKIWA KUZINGATIA USALAMA KUEPUKA AJALI

WAWEKEZAJI WA MIGODI HANDENI WATAKIWA KUZINGATIA USALAMA KUEPUKA AJALI

  • Habari
  • September 3, 2025
  • No Comment
  • 16
13 / 100 SEO Score

 

Na Mwandishi Wetu, Handeni

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amewataka wawekezaji wa migodi ya madini kuhakikisha wanazingatia kikamilifu kanuni na miongozo ya usalama ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea mgodi wa dhahabu wa GSB uliopo Kilima Mzinga, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mhe. Nyamwese amesema ni jukumu la kila mwekezaji kulinda maisha ya watu pamoja na mazingira ya maeneo wanayofanyia kazi.

Amesema Wilaya ya Handeni ina hazina kubwa ya fursa za maendeleo na kwamba mshikamano wa wananchi, wawekezaji na serikali unaweza kuigeuza kuwa kitovu cha uzalishaji, ajira na ustawi wa jamii.

Katika hatua nyingine, Mhe. Nyamwese amempongeza mwekezaji huyo kwa uamuzi wa kuwekeza Handeni, akibainisha kuwa hatua hiyo itafungua milango ya ajira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.

Aidha, ameahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na wawekezaji ili kuhakikisha changamoto za miundombinu, hususan upatikanaji wa umeme wa uhakika na maji, zinapatiwa suluhisho la kudumu.

Related post

SERIKALI YAPANGA KUIMARISHA UBORA NA USALAMA WA  CHAKULA

SERIKALI YAPANGA KUIMARISHA UBORA NA USALAMA WA  CHAKULA

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Suleiman Serera,akizungumza…
RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA HASARA

RAS ARUSHA: MAFUNZO YA PPRA YATAONDOA UWEZEKANO WA KUPATA…

11 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Bw. Missaile Musa amesema mafunzo yanayotolewa…
BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

BIL 527 ZATEKELEZA MIRADI 13 YA TANROADS TABORA-ENG MLIMAJI

16 / 100 Powered by Rank Math SEO SEO Score Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *